Friday 7 February 2014

Madhara ya Kutokujua Hali ya Afya Yako

Katika tafiti nyingi zilizofanya, iligundulika kuwa watu wengi kutoka nchi zinazoendelea hawafahamu hali za afya zao. Hii ni kutokana na kutofanya vipimo vya mara kwa mara kuangalia hali za afya.  Kwa jinsi mwili unavyofanya kazi, na jinsi ulivyo na sehemu nyingi, ni vyema tukawa na desturi ya kupima afya zetu mara kwa mara.


Sehemu Mbalimbali za Binadamu 

Sehemu hizi za mwili wa binadamu huweza kushambuliwa na magojwa mbalimbali. Na wakati mwingine ni vigumu kujua kuwa unaumwa maana sehemu iliyoshambuliwa huchukua muda mrefu kujionesha kuwa imeshambuliwa. 

Magonjwa makubwa ambayo utafiti unaonesha huharibu sana viungo vya mwili ni pamoja na Kisukari, Shinikizo la Damu, Ukoma, kupooza n.k

Inashauriwa kujenga tabia ya kuangalia afya zetu mara kwa mara ili tuweza kudundua pale tunapoumwa kabla ugonjwa haujasambaa mwili mzima.

Health Awareness Campaigns inahamasisha elimu ya afya ili jamii iweze kuwa na afya njema na kushiriki kikamilifu kujenga uchumi. Kama unalolote la kuchangia, kuuliza au kushauri tafadhali andika kwenye sehemu ya comments hapo chini.


No comments:

Post a Comment